JINSI YA KUPIGA WINDOWS KWENYE COMPUTER YAKO HATUA KWAE HATUA

KARIBUNI TECHPLATFORM LEO NATAKA KUKUONYESHA NI JINSI GANI YA KUPIGA WINDOWS 7 KWA KUTUMIA DVD KWENYE COMPUTER YAKO

JIFUNZE KUPIGA WINDOW HAPA

  Habari yako? leo nitaeleza jinsi ya kupiga window 7 kutoka kwenye cd. nifatiliee kwa makini ili uweze kupata ujuzi huu.



HATUA KWA HATUA  
Ingiza CD yako katika DVD-ROOM ya mashine yako kisha subiri CD yako isome ikisha soma Restart mashine yako kisha bonyeza Boot Button, hapa kila mashine huwa zinatofautiana ila nyingi ni F8, F10 au F12, so angalia mashine yako boot button yake ni ipi.


Kama itagoma usichoke rudia tena ila ikikubali utaona kama pichani hapo juu
Fanya machaguo sahihi hapo katika Lugha, Time na type ya keyboard hiyo kwenye picha mimi ndo huwa naitumia wakati wote sijawahi kubadilisha, kisha bonyeza Next
Utaona muonekano kama huo juu pichani sasa bonyeza Install Now
Weka tiki katika kibox ili kukubaliana na sheria za microsoft kisha bonyeza next ili kuendelea
Bonyeza Upgrade kama ulikuwa na Windows 7 na unataka kuibadilisha...Au bonyeza Custom (advanced) huna Windows 7 na unaweka windows 7 upya

Chagua Drive kama ni (C:) AU (D:) ambayo unataka kuweka windows 7.Bonyeza  Drive options (advanced) kama unataka kutengeneza Partiton (Kuigawanya hard disk ) Kisha bonyeza Next, sasa windows yako itaanza mchakato wake wa kujiweka katika mashine yako tazama picha hapa chini.




Baada ya michakato hiyo mashine yako itajizima na kujiwasha usiogope bado ipo katika mchakato tazama picha hapa chini



Ikishajiwasha itaendelea na mchakato wa setup iliyobakia itachukua muda kidogo wenda ikazidi ule muda wa mwanzo lakini usijali itamaliza kisha itajizima na kujiwasha kwa mara ya pili.






ikishawaka sasa itakupa chaguo la kuandika jina unaweza kuandika jina lolote ulipendalo pia ukipenda unaweza kuweka na Password lakini kama hautopenda andika jina tu kisha bonyeza next, wenda ikakuomba Keys chukua hapa kama hauna lakini pia unaweza kubonyeza next bila kuweka ila itakuja kukuomba baadae
Bonyeza next kisha set vitu hivi chini pichani kama utakavyopenda wewe







Mpaka kufikia hapo tayari Computer yako kwa kutumika.
 Asante
Share: 
Written by marvel tz

Post a Comment

Previous Post Next Post