jinsi ya kuingiza pesa kutumia mtandao wa whatsapp\TECHPLATFORM



Kwanza kabisa WhatsApp ilinunuliwa na mtandao wa kijamii  wa Facebook kwa dola za kimarekani bilioni 19. Ambapo baada ya hapo iliwafanya waanzilishi wa mtandao huo (Brian Acton Na Jan Koum) kuwa mabilionea. Bw. Brian anafahamika vikubwa kwa msimamo wake wa kupinga matangazo, awali alinukuliwa akisema “Watu hawaamki mapema asubuhi na kitu cha kwanza kabisa kuona kikawa ni matangazo”.

Kuchukia kwake kwa matangazo kumewezesha WhatsApp kuwa moja kati ya zile App maarufu sana ambazo hazina matangazo ndani yake.

WhatsApp wanaitumia kutengeneza pesa

Facebook Ikiwa Imeimeza WhatsApp

Bw. Brian katika akili yake alifikiria kuwa kama kampuni ikiruhusu matangazo basi kampuni itakuwa inawajali sana watangazaji kupitia mtandao huo (kwani wao ndio wanatoa pato kwa mtandao) kuliko watumiaji wa mtandao huo kama wewe na mimi .

Baada Ya Kusema Hayo, Naomba Nianze Kulijibu Kama Ifuatavyo.

Swali moja ambalo linawasumbua watu wengi ni jinsi gani mtandao huu wa WhatsApp unaingiza pesa?

Watu wengi hawalijua hili lakini mtandao huu wa WhatsApp una timu ndogo sana (ukilinganisha na makampuni mengine kama vile Facebook na Twitter). Timu nzima ya WhatsApp ina watu 50 tuu, yaani hawa ndio watu nyuma ya huduma nzima ya WhatsApp. Timu hiyo inawawezesha watu duniani kubadilishana meseji bilioni 50 kwa siku. Sasa kwa nini hii ni muhimu?

WhatsApp imeruhusiwa na wakubwa wake (Facebook) kuwa na timu ndogo na timu hiyo haihusishi watu wa masoko, utangazaji kwa kuwa wanayachukia matangazo na pia hawana watu wanaohusika na mauzo. Timu ya watu waliyonayo ni wale wakuzaji (developers) tuu na mara kwa mara huwa wanachagua mtu au watu wa kuwashauri kwa mda tuu.                                

Sasa kama timu nzima ina watu 50 tuu, basi kutakuwa hakuna nguvu kubwa sana kuhakikisha kampuni hiyo inaishi sio?. Kwa sasa WhatsApp bado inatoza chaji kwa baadhi ya maeneo katika dunia ambayo yanawapatia mamilioni ya dola kwa mwaka.

Lakini ukifuatilia sana utaona kuwa wapinzani (wa kibiashara) na WhatsApp wanatoza wateja wao kwenye mauzo ya ‘Emoticons’ na pia wanaonyesha matangazo ambayo yanawapatia mamilioni ya dola kuliko mtandao wa WhatsApp.

Swali lingne la msingi linakuja sasa, Hivi ni kwanini Mark Zuckerberg alilipa dola bilioni 19 za kimarekani katika kununua mtandao ambao huataenda kumtengenezea pesa nyingi?.

Jibu ni kwamba watu hawaonyeshwi matangazo lakini kumbuka ukishakuwa na kundi la watu katika sehemu moja hizo zinakuwa kama ni data. Taarifa (Data) za mamilioni na mamilioni ya watu duniani zinakusanywa na kuuzwa na pia zinatumika katika mtandao wa Facebook kama njia yao katika matangazo wanayoyaruhusu katika mtandao wao.

Utangazaji wa Facebook uko vizuri katika kujua ni watu gani wa kufikiwa na matangazo hayo.Taarifa (data) kama hizi zinapatikana katika mtandao wa WhatsApp na Facebook inazitumia taarifa hizi vizuri sana.Kwa harakaharaka ni kwamba mtandao wa WhatsApp unatumika kama kituo cha kukusanya taarifa ambazo zitakuja kuwa na mfanikio makubwa kwa mtandao wa kijamii wa Facebook



Mpaka hapo natumai umeshajua ni jinsi gani jamaa wanatengeneza pesa sio? Kumbuka hakuna cha bure tena kikawa kizuri vile. Usije ukashangaa WhatsApp wakabadilisha misingi yao na kuanza kuonyesha matangazo kwani wapo chini ya Facebook na lolote linaweza likatokea.

Post a Comment

Previous Post Next Post