Akizungumza leo,Julai 28,mwaka 2021,katika Mkutano wa mapato na matumizi ya Wizara hiyo ,Waziri wa Wizara hiyo Dk.Faustine Ndugulile amesema wamepata taarifa kuna namba ambazo bado zinaendelea kuwatapeli watu hivyo mpaka sasa wamefungia laini hizo za simu 18,622 ambazo zilikuwa zikitumika kuwatapelia watu mbalimbali.
Amesisitiza kwamba wamepata taarifa kuna namba zinaendelea kufanya uhalifu,hivyo wapo makini na wataendelea kuchukua hatua."Tupo very serious tumeshafungia laini 18,622 kuanzia Aprili mpaka Juni mwaka huu.Sambamba na hilo namba zote ambazo zilifanya utapeli huo tumezizua vitambulisho vilivyotumika kusajilia laini 14768.
“Niwaombe watanzania kuendelea kufanya uhakiki wa laini zetu ili haya yasitokee kwani watu wamesajiliwa na tutawafungia laini kazi hii tunaifanya,Sasa tunaenda kuwatafuta ili tuwafungulie mashtaka tupo Serios katika hili,”amesema.
Aidha,Waziri Ndugulile amewataka watanzania kuendelea kuhakiki namba zao kwani zaidi ya watanzania milioni 10 bado hawajahakiki laini zao.“TCRA walikuwa wanatoa taarifa ya nusu mwaka kuhusiana na masuala ya uhalifu na kama tunavyokumbuka tulitoa maelekezo ya usajili wa laini kila mtu ahakiki zoezi hili linaenda vizuri lakini bado watanzania wengi zaidi milioni 10 hawahakiki."
Ametumia nafasi hiyo kuwaomba kuhakiki kwani utaratibu ni rahisi tu na kwamba huo mchakato utaendelea huku akisisitiza wataanza kuzizima laini ambazo hazikuhakikiwa ."Kufanya uhakiki wa laini yako hauhitaji kusumbuka kwenye simu yako unaweza kufanya uhakiki na utaona laini zote zilizosajiliwa,”amesema
Pia,Waziri huyo amesema tangu Wizara imeanza miezi saba iliyopita wameweka mikakati ya ufuatiliaji wa karibu kila baada ya miezi mitatu wana vikao vya kufanya mapitio ya malengo ambayo wamejiwekea, mapato na matumizi lengo ni kujipanga kuifanya kazi vizuri.
“Katika mkutano tumeona mwelekeo wetu ni mzuri kwani taasisi tunazosimamia zimeanza kutekeleza na hali ya utekeloezaji wa malengo ni mzuri na mapato yanaenda vizuri lakini pia tumweza kubana matumizi ili tuendeshe kwa faida,Tumefanya maboresho makubwa TCRA,”Dkt.Ndugulile amesema.
SERIKALI YAFUNGIA LAINI ZA SIMU 18,622 ZILIZOKUWA ZIKITUMIKA KUFANYA UTAPELI
SERIKALI kupita Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, imesema katika kipindi cha Aprili hadi Juni mwaka huu jumla ya laini za simu 18,622 ambazo zilikuwa zikitumika kuwatapelia watu zimefungiwa huku ikigundua vitambulishi 14,768 vilitumiwa na matapeli kusajili laini hizo.
Kaimu Postamasta Mkuu Bw. Macrice Mbodo,,akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mapato na matumizi ya wizara hiyo na taasisi zake kilichofanyika leo Julai 28,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile akiwa na Naibu wake Dkt Zainab Chaula wakifatilia mada mbalimbali wakati wa Mkutano wa Mapato na matumizi ya wizara hiyo na taasisi zake kilichofanyika leo Julai 28,2021 jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Justina Mashiba (kulia),Kaimu Postamasta Mkuu Bw. Macrice Mbodo (katikati) pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu TTCL Bw.Vedastus Mwita (kushoto) wakafatilia mawasilisho mbalimbali wakati wa kikao cha Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile cha kujadili Mapato na matumizi ya wizara yake pamoja na taasisi zake kilichofanyika leo Julai 28,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia kikao cha majadiliano kuhusu Mapato na matumizi ya wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na taasisi zake kilichofanyika leo Julai 28,2021 jijini Dodoma.
Tags:
SIMU