FAHAMU KULINDA SIMU YAKO ISI ARIBIWI NA MTU MWINGINE

Simu yako, hasa simu-janja ni muhimu sana. Simu hizi za kisasa zinabeba taarifa nyingi, zikiwemo taarifa nyeti. Jambo la kwanza na la muhimu ukimiliki simu ya aina yoyote ni kuwa na uelewa mzuri wa kuidhibiti na kulinda taarifa zako zilizomo kwenye hiyo simu.


Taarifa zako zinaweza kuwa namba za simu, akaunti zako za mitandao, nyaraka, sauti, picha na video. Taarifa inaweza kuwa chochote, hauwezi kujua mtu mwingine anaweza kutumia taarifa ya aina ipi kukuvuruga.
 

1. Weka Mlango wa aina Yoyote Unaohitaji Siri

Kanuni ya kwanza ya kujisitiri ni kuweka mlango wa kuingilia kwenye simu yako ambao ufuunguo wake unao wewe tu. Fanya hivi kwa kuweka namba ya siri (PIN), alama (pattern) ya siri, ufahamu wa uso (‘face recognition’) au hata alama ya kidole (touch ID)  kwa simu za hali ya juu.

Weka Mlango wa Kuingilia kwenye simu yako kuzuia mtu kupata data zako hata kama akiweka simu kwenye kompyuta

Kwa nini?
– Kutunza taarifa iwapo simu ikipotea au kuibiwa.
– Kuzuia mtu kuangalia data hata inapochomekwa kwenye kompyuta, hususani ikiibiwa.
– Hakikisha data za nyeti huweki kwenye sd-card. Zikijaa kwenye simu hamisha kwenye kompyuta.
– Kuzuia mtu kuformat simu kuformat simu kwa mzaha au kisasi.
– Unaweza kuweka taarifa za mmiliki ili simu ikipotea, mtu anaweza kutumia taarifa ulizoweka kukutafuta.
SOMA PIA  Apple kufanya uzinduzi wa tofauti sana Machi 27
 

2. Toa Mcharazo wa Alama ya Kufungua Simu
Unashauriwa kwamba kama hauna matatizo yoyote ya macho, toa kabisa mfuatilizo wa alama (pattern) ili mtu wa nyuma yako au karibu, kwenye sehemu za kadamnasi asione pasiwedi yako. Watu wengi wanakosea kutofanya hili. Angalia picha hapa chini kuweza kuficha mcharazo.
make pattern invisible
Kuficha ‘pattern’, ingia kwenye ‘settimgs’->> Lock Screen. Kwenye ‘Make Pattern Visible’, hakikisha hii huduma haijawekewa alama ya tiki.
 

3. Unga Simu na Huduma ya Kutafuta simu
Jambo la tatu hapa unaloshauriwa ili kudhibiti simu yako ni kujiunga na huduma ya kutafuta simu yako. Huduma hizi ni pamoja na Android device manager, Apple i-Cloud, Windows find my phone, Avast Free Mobile Security na nyingineo ambazo hutumia ramani kutafuta simu yako iliyoibiwa iwapo tu ikiwashwa na kujuiunga na intaneti.
SOMA PIA  VOLVO kuyajaribu magari yanayojiendesha UINGEREZA

Kuhusu kutafuta simu yako ya Android, angalia makala hii ->> Mbinu Ambazo Pengine Hujui Google Play
 

4. ‘Encrypt’ Simu yako
 Kui-'encrypt' simu yako, ingia kwenye 'settings' ->> 'Security na chagua 'Encrypt Device'. Itachukua muda kidogo, kwahiyo hakikisha simu yako ina chaji ya kutosha.
Kui-‘encrypt’ simu yako, ingia kwenye ‘settings’ ->> ‘Security na chagua ‘Encrypt Device’.
Itachukua muda kidogo, kwahiyo hakikisha simu yako ina chaji ya kutosha.
Encryption’ ni namna ya kuficha taarifa ndani kitumi.
Watu wengi huamini kwamba wakishafanya ‘reset’ basi data zao zinakuwa zimefutika na hivyo kuweza kuuza simu wakiwa salama. Hii sio sawa. Data zako zinaweza kupatikana tena kwa ujanja mdogo tu kama una muda. Kwa ajili ya kuhakikisha kwamba data zako haziwezi kupatikana kabisa, tumia encryption.

Simu ikifanyiwa Encryption, itahiji pasiwedi ya ziada punde inapowashwa. Pia mtu hawezi kupata data za hiyo simu hata kama ana ujuzi wa ndani wa kompyuta na akaiflash simu hiyo.
 

5. Tumia App za faragha.
Katika Maisha ya kawaida, mtu anaweza kukuomba kufanya kitu, kumbe anataka kufanya kitu kingine. Kama wewe ni mtu wa watu, kutumia app za fragha kutakusaidia sana.
Mbinu hii itakusaidia kuongeza milango mingine ya kulinda app zako ili kuzuia mtu asiingie kwenye sehemu unazohitaji faragha. Moja ya app maarufu za faragha kwa android na windows phone ni AppLock
 

6. Tumia cover na screen protector
Mbinu ya mwisho hapa ni kutumia kasha (au kava au ‘cover’) kujisitiri ukiwa kwenye kadamnasi. Kuna aina nyingi ya za ila kava ya kujisitiri (au ukiulizia ‘privacy cover’) ndio inayozungumziwa hapa. Kava kama hizi zinapunguza mwanga unaoonekana kwa mtu wa pembeni ili asione unachofanya kwenye simu. Nunua cover ya plastiki inayoganda kwenye skrini ili Isichubuke au kwa bei ya juu kidogo, unaweza kununua kava ya kioo kizuri

Post a Comment

Previous Post Next Post