Adf.ly ni site ambayo inamruhusu mtu kufupisha link ndefu kuwa fupi kama vile http://bongotechno.blogspot.com kuwa http://adf.ly/1gdeMw , Sio tofauti sana na bit.ly, tinyurl.com au goo.gl . Hata hivyo Adf.ly iko tofauti na hizo kwa sababu Adf.ly wanaweka matangazo yao katika hizo link,
Yani hivi: Pindi mtu akifungua link iliyofupishwa na Adf.ly kutakuwa na tangazo kwanza ambalo linakuwa kwa sekunde 5 kisha mtu atapeleka katika link husika. Mfano: facebook.com itakuwa http://techplatform6.blospot.com Hivyo mtu kabla ya kupelekwa facebook litatokea tangazo kwanza kwa sekunde 5 kisha atapelekwa Facebook.
Jinsi Adf.ly inavyofanya kazi
Adf.ly sio tofauti sana na bit.ly au goo.gl tofauti yake ni kwamba adf.ly kunakuwa na matangazo katika link zao, Adf.ly inafanya kazi pale mtu akifupisha link yake kisha akaipost facebook, twitter au kwenye forums kisha mtu akija kuclick ile link ambapo litatokea kwanza tangazo na kisha huyo mtu akiliangalia kwa sekunde 5 kisha akapelekwa kweenye link husika basi wewe utalipwa au mfano bofya hii link ya http://facebook.com iliyofupishwa kuwa http://adf.ly/1gdeMw.
Kwa kifupi
Mtu akiliangalia tangazo kwa sekunde 5 kisha akapelekwa katika link husika basi wewe utalipwa
Kiasi gani naweza kutengeneza na Adf.ly?
Adfly wanalipa dola 0.5 hadi dola 9 kwa kila views 1000 ,
(Inategemea na Nchi husika)
NB:
Facebook ina watumiaji takribani milioni 500 kwa siku, Hivyo hukosi kupata Click 1,000 kwa siku, Unaweza ukapost link zako kwenye magroup ya Facebook ili kupata click nyingi
Malipo yanakuwaje
Adf.ly wanalipa kiwango cha chini kuanzia Dola 5, Hivyo kama ukifikia dola 5 basi watakulipa automatically kwenye akaunti yako ya PayPal, Payoneer au Payza (Kwa Tanzania tumia Payza au Payoneer ) .
Jinsi gani kutengeneza pesa kutoka Adf.ly?
Kitu kikubwa ambacho nakipenda kutoka Adf.ly ni kwamba hata mtu ambaye hana blogu au hana ujuzi wowote kwenye internet naye anaweza kutengeneza pesa. Hakuna ujuzi wowote unaohitajika ili kujipatia kipato kutoka Adf.ly. Ili uweze kujiingiza kipato kutoka adf.ly unatakiwa kushare link zako ili upate click katika hizo links.
KUMBUKA
Mtu ataclick link yako kama akivutiwa na hicho kitu , hivyo weka link za vitu vinavyowavutia watu.Hizi ndio sehemu ambazo unaweza ukashare links zako .
1. Facebook.com
Mamilioni ya watu wanatumia Facebook kila siku, Hivyo Facebook ni sehemu bora ya kupost links zako na kupata watu wa kuclick hizo links.
2. Twitter.com
Ukiwa na followers wengi twitter unaweza ukapost links zako ili follower wako wa click hizo link
3. Youtube.com
Pia unaweza ukatumia Youtube.com kuweka link zako kwenye maelezo ya video
4.Forums
Kuna forum nyingi ambazo zinaruhusu kuweka link, hivyo unaweza ukapost link zako kwenye forums
Blogu au website
Kama una blogu au website unaweza ukaweka link zilizofupishwa na Adf.ly au hata kama hauna website unaweza kucomment link kwenye blogu .
Hivyo kwa kutumia Adf.ly utaweza kujiongezea kipato kwa urahisi zaidi
Jiunge nao kwa kubofya