Sasa hivi simu janja za kujikunja ni nyingi mno na kwa sasa teknolojia hii kwa kiasi kikubwa imeanza kuzoeleka
Tumeshaandika sana kuhusu simu na vifaa mbali mbali vinavyotumia teknolojia ya kujikunja HAPA, pitia kwanza kidogo.
Taarifa zilizopo ni kwamba Kampuni ya Apple inatumia teknolojia ya OLED ambayo imetumiaka katika Samsung Galaxt Z Fold 3 ambayo inasemekana ndio teknolojia kubwa katika simu za kujikunja kwa sasa.
Hii inaonekana ni hatua moja wapo katika kuhakikisha kuwa kampuni inatengeneza iPhone, iPad, au hata Mac ya kujikunja (lakini jicho letu kwa sasa lipo kwenye iPhone).
K
umbuka kitu kimojawapo kinachofanya teknolojia hii makampuni mengi kushindwa ni kwamba ni vigumu sana kufanya kioo kikawa na wembamba unaotakiwa kuweza kujikunja hata kwa miaka kadhaa mbeleni.
Teknolojia ambayo Samsung wameitumia katika Samsung Z Fold 3 mpaka sasa imeonekana ikifanya vizuri tuu na pengine ndio sababu husika Apple nao wakaona wasibakie nyuma.
Mpaka sasa hizi ni taarifa tuu ambazo zipo na haijulikani muda ambao Apple watazalisha kifaa kutoka kwao ambacho kinajikunja ambacho pia kitatumia teknolojia hii.