MAMBO 5 YAKUYA EPUKA UNAPOANZA BIASHARA YA MTANDAONI|tech platform


KARIBU KWENYE WEBSITE YAKO PENDWA YA TECH PLATFORM NA LEO NITAKUJUZA MAMBO 5 YAKUYA EPUKA UNAPOANZA BIASHARA YA MTANDAONI

http://techplatform6.blogspot.com   

Somo hili ni muhimu kwasababu ukiweza kufahamu makosa haya na kuyaepuka basi ni rahisi biashara yako unayofanyia mtandaoni kukutengenezea pesa.

Kwanza kabisa niseme Internet imetoa nafasi kubwa kwetu sisi wajasiriamali kuweza kufikia idadi kubwa ya watu wakuwauzia bidhaa au huduma tunazotoa. Kwa maana hii iwapo utafahamu namna yakutumia nafasi hii vizuri basi bila shaka utatengeneza cash 💰

Jambo muhimu ni kufahamu nini unachofanya.

Sasa basi tutazame makosa 5 yakuepuka unapoendesha Online business.

1 • Kutochukulia business seriously.

Ndiyo.




Watu wengi wanaoanza online business hawachukulii kwa umakini business zao wakati wanaanza.

Wengi wanaona ni kama hobby tu kwahiyo hata nisipofanya leo nitafanya kesho. But you know what?

Time is no good friend.

Muda mrefu utapita na business yako haitaenda popote.

Kwahiyo hapo unaona. Unahitaji kuwa serious.

Jitahidi kuwa serious utengemda kwaajili ya business yako hata 10 minutes kwa siku.

Fanya hiyo katika consistency manner.

Kila siku.

2 • Kutoelekeza nguvu kwa wateja.

Ok.

Here is the deal.

Ukitaka business yako ikutengenezee pesa lazima u-focus kwa vitu wajeja wanataka.

Unajua wakati unaanza online business unahisi kama vile hiyo biashara ni kwaajili yako.

But you are wrong.

Biashara ni kwaajili ya wateja.

Kama hautokuwa tayari kubadilika na kuendana na wateja wanachotaka basi hiyo biashara yako itabaki ya kwako na kamwe hutoweza kutengeneza pesa.

Simple as that.

Hii Point ni muhimu sana kwasababu watu wengi wanaoanza online business wanadhani wanachopenda wao Katika biashara waliyoanzisha basi na wateja nao watapenda hivyo.

Nop.

Wateja wanajua nini wanachohitaji.

Kwahiyo ni muhimu sana kuwekeza nguvu kufahamu wateja wanavyotaka uwahudumie na uwe tayari kubadilika mpaka pale unapopata “market fit”

Hiyo maana yake sasa umeshapata soko lako, unauelewa na wateja wako na pia jinsi wanavyotaka kuhudumiwa.

Ukifanya hivyo you will make millions.

3 • Kutokuwa online muda mwingi.

Yep.

Unakuta mtu anaanza online business lakini hayupo Online wiki moja au mbili.

This is a joke.

Kwa mfano mtu unamtumia Email kwaajili ya business anajibu baada ya wiki.

Huwezi kupata pesa kwa namna hii.

Ili uweze kuunda kweli online business inabidi uwe active mtandaoni.

Hii itakuwezesha kuwasiliana na potential clients wako kwa haraka.

Na ukifanya hivi utaongeza ushawishi kwako.

Ukiongeza ushawishi kwao inamana utaweza kufanya nao biashara.

Anza leo kuwa active kwenye biashara yako ya mtandaoni na hakika utaona improvements.

Be organized.

Jiwekee kanuni kwamba kila siku lazima ufanye jambo fulani kwaajili ya business yako.

Don’t be lazy.

You need to grind to make money online.

4 • Kutofanya Uchunguzi kabla yakuanza Online Business.

Hapa swali muhimu kabisa ni...

Je, bidhaa au huduma unayotaka kuanzisha ina wateja?

That is a million dollars question.

Kufahamu kwa undani biashara unayotaka kuanza ni muhimu.

Lakini haiishii hapo.

Unatakiwa pia ufahamu je kuna wateja wakutosha wakununua bidhaa au huduma yako?

Kwasababu unaweza tumia muda mwingi na fedha kubuni na kuanzisha biashara isiyokuwa na wateja.

Na nikwambie tu watu wengi wameingia katika mtego huu.

Walitumia muda mrefu na fedha nyingi lakini mwisho wa siku wakagundua hakuna soko lakutosha kuuza bidhaa zao.

Hiyo ni hasara na pia muda ulipotea haurudi.

Katika kipengele hiki nasisitiza sana kufanya research.

Talk to people who are in the same industry and learn from them.

Utaokoa muda na pia utajifunza aina gani hasa ya Online business inaweza kukutengenezea pesa na si kufanya kwa kubahatisha.

5 • Kutokufanya Marketing & Advertising.

Watu wengi wanaonza online business wanadhani wataweza kuwafikia wateja na kuuza bila kuweka mkazo mkubwa kwenye marketing & advertising.

Nikwambie tu huwezi kuuza bila kuwajulisha potential customers kuhusu biashara yako.

Na unaweza kuwajulisha Kuhusu biashara yako kwakutumia Email Marketing, Facebook Advertising, Google Ads, Instagram Ads na YouTube.

Kutumia huduma hizi za kutangaza biashara yako itabidi uwekeze pesa.

And it is not that much.

Tatizo la watu wanaoanza online business hawataki kuwekeza kwenye biashara zao wenyewe.

Na hapo ndipo wanakwama.

Mwisho wa siku......guess what?

They quit.

Nikuambie tu pesa inaenda kule pesa ilipowekezwa.

Usione hatari kutumia pesa kutangaza business yako.

Ukitangaza vizuri Business yako itakuja kukutengenezea faida millions time ukilinganisha na kiasi ulichotumia kwenye matangazo.

Ok...

Ngoja niishie hapa kwa leo.

Tukuatane siku nyingine kwaajili ya somo jingine muhimu katika eneo hili la making money online.


Post a Comment

Previous Post Next Post