Kuna mdau amenifanya niandike hiki nachoenda kuandika kwa sasa, Ahsante sana kwa kunifanya nipate jambo la kushare na wadau wangu kupitia huu ukurasa wangu Leo nataka nikupe tu njia rahisi ya kutoa iCloud lock kwenye simu za iPhone 6 5s 5c 5 4s 4. kumbuka kuwa unapokumbana na tatizo la icloud lock ni dhahiri kuwa unakuwa huna uwezo wa kutumia kiaa chako, na hii inatokea pale ambapo unakuwa umesahau password zako au pale napo kuwa umenunua simu used kupitia kwa mtu au hata kwenye mitandao, ipo mitandao mingi sana inayouza vitu online ila nisingependa kuitaja hapa.
kuna njia mbili za kuweza kutoa icloud lock kwenye simu hizi
NJIA YA KWANZA
Ni kwenda kwenye store yoyote ya Apple iliyo karibu na wewe huku ukiwa na ushahidi wa kutosha kutoka kw mmiliki wa simu ambaye amekuuzia. mfano kama mliandikishiana au kama ulinunua mtandaoni basi ni vyema ukaenda na risiti ili kuthibitisha umiliki wa hiyo simu kutoka kwa aliye kuuzia. hii ni njia rahisi sana kwani kinachotakiwa ni uthibitisho tu. tatizo kubwa linalo jitokeza katika njia hii ni kwamba wengi wetu hupenda kununua simu za mikononi na pia si watunzaji wa risiti
NJIA YA PILI
Kama njia hiyo hapo juu imeshindikana basi njia nyingine ya kutoa hizo lock ni kufanya kitu kinachotwa Bypass iCloud Account activation Lock and Disable iCloud Lock screen
hivyo basi ili kufanya njia hii fata maelezo haya
angalia aina ya simu unayo tumia mfano iphone 4s
baada ya hapo nenda sehemu ya kupigia simu kisha piga *#06# utaletewa imei number za simu yako kisha zicopy pembeni
baada ya hapo nenda kwenye website ifuatayo Official iCloud Activation Lock Removal
jaza taarifa zako kama ifuatavyo
Handset type: chagua saina ya simu unayotumia mfano iphone 4s
IMEI/Serial: hapo jaza imei za simu yako ambazo ulikuwa umezicopy pembeni
kisha bonyeza add to cart kisha itafunguka page itakutaka uhakikishe na kuingiza email yako
huduma hii ni ya kulipia na inagharimu £ 19.99 na inachukua siku 1 hadi tatu
baada ya muda utapokea email itakayo kujulisha kuwa Activation Lock zimeondolewa kwenye simu yako
baada ya hapo utahitajika kutengeneza account ya kwako ya icloud ya find my phone huku ile ya mara ya kwanza itakuwa imeondolewa kabisa
njia hii inaweza kutumika kwenye iphone zote pamoja na ipad pia. kumbuka njia hii sio ya bure ni njia ambayo inatumia gharama
Tags:
MAUJANJA