Simu janja zimekuwa msaada kwetu kwa mambo mengi ambayo zimekuwa zikirahisisha shughuli kadha wa kadha kwenye ulimwengu huu wa teknolojia. Ile taa ya kuongeza mwangaza pembeni ya kamera ya nyuma ni tochi pia ambayo unaweza kuiwasha kiurahisi kabis
Uwepo wa taa pembeni ya
kamera imekuwa na kazi zaidi ya moja
na wale ambao tunapenda
kuongeza ubora wa picha kabla
ya kupiga ama inatokea upo
sehemu yenye mwanga hafifu na
unahitaji msaada wa kuona kitu
fulani vizuri hakika tunashukuru kwa
simu janja zetu kuwa na kitu
ambacho kimewekwa kwa ajili
ya kazi hiyo.
Sasa inatokea wakati fulani unatamani upate wepesi wa kuwasha/kuzima tochi au kamera bila ya kufuata hatua ambazo sote tunazifahamu lakini inakuwa haiwezekani. Changamoto inapotokea ndio inakuwa chachu ya kutafuta jibu la kitu fulani na kutokana na ukuaji wa teknolojia suala zima la kuwasha ama kuzima iwe tochi au kamera ni rahisi kabisa.
Fahamu kuhusu Shake Flashlight & Camera
Shake Flashlight & Camera ni programu tumishi inayopatikana kwenye Playstore ikiwa imetengenzwa kumwezesha mwenye simu janja ya Android kuwasha/kuzima tochi au kamera kwa kuitikisha tu kwa mara kadhaa. FUata hatua hizi ili uwe unaweza kuwasha na kuzima kamera/tochi kwa urahisi sana:
>Mara baada ya kupakua programu tumishi husika (Shake Flashlight & Camera) ifungue na utauona ujumbe utaojitokeza kuhusu matumizi ya betri kwenye programu tumishi hiyo. Unaweza kuchajua Cancel kwa maana ya kuupuzia kile kilichoelezwa au ukachagua “Don’t show again” na kubofya “Disable“.
Hatua ya pili ni kuwasha kitufe (kupeleka upande wa kulia) kwa maana ya kuruhusu (on) kwenye kipengele cha tochi (Flashlight). Halikadhalika, utafanya hivyo hivyo iwapo utapenda pia kuwasha kamera kwa kuitikisha tu.