Unakumbuka nini katika Nokia 3310, Nokia 3310 vs iPhone 12 Pro Max|TECH_PLATFORM©

 



Binafsi NOKIA 3310 inanikumbusha nyakati nzuri, nikiwa mdogo. Mzee wangu alikaa na hii simu kwa muda mrefu sana. Simu mpya zilikuja na zikaondoka yeye yumo tu. Hadi nilianza kutamani ipotee!

Nokia iliwahi kuwa brand yenye simu bora zaidi duniani. Simu zake zilisifika kwa ubora na hasa ugumu wake. Enzi hizi Nokia walikuwa wanajaribu kila design ya simu, yani idea ikija wanatoa tu simu


Bahati mbaya kwa Nokia, ni kampuni ya kizungu, kutoka Finland. Simu zao hazikubamba sana Marekani na hivyo baada ya muda waliishiwa upepo. Licha ya Nokia kutoa simu nyingi, NOKIA 3310 ndiyo ilibamba sana ukanda wa Afrika na Asia. Leo tunafanya utani kidogo kulinganisha NOKIA 3310 na simu mpya ya Appla iPhone 12 Pro Max. Ungenunua ipi?

ASANTE KWA KUSOMA PIA UNA WEZA KUPATA MAUDHUI MENGI KWA KUJIUNGA NASI YOUTUBE FACEBOOK GOOGLE

Post a Comment

Previous Post Next Post